Hamia kwenye habari

DESEMBA 20, 2019
ARGENTINA

Buenos Aires, Argentina—2019 Kusanyiko la Kimataifa la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

Buenos Aires, Argentina—2019 Kusanyiko la Kimataifa la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
  • Tarehe: Desemba 13-15, 2019

  • Mahali: Estadio Único de La Plata, Buenos Aires, Argentina

  • Lugha ya Programu: Lugha ya Ishara ya Argentina, Kiingereza, Kihispania

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 47,555

  • Idadi ya Waliobatizwa: 563

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,300

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Amerika ya Kati, Bolivia, Chile, Czech-Slovak, Finland, Hispania, Italia, Korea, Marekani, Paraguai, Peru, Romania, Skandinavia, Ulaya ya Kati

  • Mambo Yaliyoonwa: Mara Anapios, msimamizi wa mauzo katika hoteli ya Panamericano ambamo wajumbe walikaa, alisema hivi: “Katika wakati kama huu ambapo kuna migogoro ya ndani kwa ndani, kati ya nchi fulani, na duniani pote, ninahisi kwamba matukio kama haya ni muhimu sana kwa kuwa ni mfano mzuri wa undugu, amani, na upendo, mambo ambayo tunayohitaji kwelikweli.”

 

Ndugu na dada wenyeji wakikaribisha wajumbe katika uwanja wa ndege

Ndugu wanne waliowakilisha Mashahidi wa Yehova wakizungumza na waandishi wa habari kabla ya kusanyiko

Ndugu na dada wakiingia kwenye uwanja wa kusanyiko

Wahudhuriaji wakipiga makofi kusanyikoni baada ya programu

Ndugu wapya wakibatizwa kwenye moja ya vidimbwi vitatu kusanyikoni

Ndugu Kenneth Cook, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya Jumapili

Kikundi cha akina dada kikipiga picha na herufi nne zinazouunda maneno “LOVE” yaani “UPENDO”

Wajumbe waliovalia nguo za kiasili wakipiga picha pamoja

Watumishi wa wakati wote kutoka nchi mbalimbali wakiwapungia wasikilizaji mkono baada ya programu ya Jumapili

Ndugu wenyeji wakicheza jukwaani katika tafrija ya jioni kwa ajili ya wajumbe