Hamia kwenye habari

Kushoto: Jumba la Ufalme lililoharibiwa na kimbunga. Kulia: Ramani inayoonyesha eneo lililoathiriwa na kimbunga

MEI 28, 2020
FILIPINO

Msimu wa Dhoruba Nchini Filipino Waanza kwa Kimbunga Vongfong

Msimu wa Dhoruba Nchini Filipino Waanza kwa Kimbunga Vongfong

Mei 14, 2020, Kimbunga Vongfong (kinachoitwa Ambo nchini Filipino) kilipiga kisiwa cha Samar. Kimbunga hicho ndicho cha kwanza kutokea mwaka wa 2020 katika Bahari ya Pasifiki Magharibi. Upepo uliovuma kwa mwendo wa kilomita 185 kwa saa ulipiga eneo la Samar. Mamia ya maelfu ya watu waliokolewa kutoka katika eneo hilo, na ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa serikali iliagiza kwamba kila mtu azingatie kukaa umbali unaofaa kutoka kwa mwenzake kwa sababu ya ugonjwa wa corona.

Ingawa hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa, 59 kati yao walilazimika kuhama kutoka nyumbani kwao. Walikaa katika shule zilizokuwa zikitumiwa kama mahali pa kukimbilia, au katika nyumba za Mashahidi wenzao. Mbali na hilo, nyumba za akina ndugu 82 ziliharibiwa. Pia, Majumba matano ya Ufalme yaliharibiwa kwa kadiri kubwa, na moja lilibomolewa kabisa. Ofisi ya Tawi ya Filipino imefanyiza Halmashauri mbili za Kutoa Msaada ili kushughulikia mahitaji ya kimwili na ya kiroho ya ndugu na dada walioathiriwa.

Tunaendelea kusali kwa ajili ya ndugu zetu nchini Filipino ambao wanakabiliana na majanga hayo mawili kwa wakati mmoja, kimbunga na ugonjwa wa corona. Tuna uhakika kamili kwamba Yehova, ‘Mwamba wetu wa milele,’ ataendelea kushughulikia mahitaji yao.—Isaya 26:4.