Hamia kwenye habari

ISRAEL

Maelezo Mafupi Kuhusu Israel

Maelezo Mafupi Kuhusu Israel

Historia ya Mashahidi wa Yehova katika Israel ya leo imeanza tangu mwaka wa 1920, na kwa ujumla wamefurahia uhuru wa ibada. Shirika la Mashahidi wa Yehova nchini Israel lilisajiliwa kisheria mwaka wa 1963 na 2000. Mashahidi walituma maombi ya usajili rasmi ili kuwa shirika la kidini mwaka wa 2000 na 2014, hata hivyo bado maombi yao hayajakubaliwa.

Sheria nchini Israel inaruhusu vikundi vyote vya kidini kutangaza imani zao hadharani. Hata hivyo, wafuasi wa vikundi vya washikilia imani kupita kiasi wa dini za Kiyahudi wamewapinga, wamewanyanyasa, kuwatendea kijeuri Mashahidi.

Washikilia imani hao wa kupita kiasi wamefanikiwa kwa kiasi fulani kuwashawishi maofisa wa serikali kuwanyima Mashahidi haki zao kama vile haki ya kukusanyika. Manispaa zinapokataa kuwapa Mashahidi kibali cha kukusanyika ili kufanya mikutano katika majengo ya umma, Mashahidi wamefungua mashtaka katika mahakama za rufaa ili kushughulikia mambo hayo. Mahakama ya Wilaya ya Haifa (katika mwaka wa 2007) na Mahakama Kuu (katika mwaka wa 2015) zimekubali kwamba maamuzi ya manispaa hizo yaliwabagua Mashahidi kwa sababu za kidini. Mahakama iliamua kwamba Mashahidi wana haki ya kukutana pamoja kwa amani bila kufanyiwa vurugu. Pamoja na hayo, bado Mashahidi wa Yehova wanaendelea kubaguliwa.