Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HABARI KUU | NI NINI CHANZO CHA MAMBO YA UCHAWI?

Kuvutiwa na Mambo ya Uchawi!

Kuvutiwa na Mambo ya Uchawi!

‘Burudani zinazohusisha utendaji wa roho waovu au pepo, zinachukua mahali pa wahusika wa kubuniwa kama vile wanyonya damu, mbweha-watu, na mizuka.’—The Wall Street Journal.

WACHAWI wakubwa kwa wadogo, wachawi wenye ushawishi, na wanyonya damu wenye sura za kupendeza, ni baadhi ya wahusika wenye uwezo usio wa kawaida ambao wanatumiwa katika vitabu, sinema, na michezo ya video. Kwa nini mambo hayo huwavutia watu wengi?

Profesa wa masuala ya jamii, Claude Fischer aliandika hivi: “Uwiano wa watu wanaoamini mizuka nchini Marekani umeongezeka katika miaka ya karibuni, kutoka mtu mmoja kati ya kumi hadi mtu mmoja kati ya watatu. Idadi ya vijana nchini humo ambao wamewahi kuwasiliana na wabashiri, wanaoamini utendaji wa pepo, au wanaoamini uwepo wa nyumba zenye majini, ni mara mbili ya watu wazima wanaoamini mambo hayo.”

Haishangazi kwamba, masimulizi kuhusu watu wenye roho waovu yameanza kurudi tena kwa kasi. Katika jarida la The Wall Street Journal, Michael Calia aliandika hivi: “Kuibuka upya kwa habari zinazohusu watu kuwa na roho waovu katika jamii kumesababishwa na kuenea kwa masimulizi ya mizuka, mbweha-watu, na wanyonya damu katika miaka ya nyuma.”

Ripoti moja ilisema hivi: “Asilimia 25 hadi 50 ya watu ulimwenguni pote wanaamini kuna mizuka, na mizuka ni maarufu sana kwenye vitabu katika tamaduni nyingi.” Utafiti uliofanywa nchini Marekani na maprofesa wa masuala ya jamii Christopher Bader na Carson Mencken “ulionyesha kuwa asilimia 70 hadi 80 ya Wamarekani wanaamini angalau aina moja ya utendaji unaopita uwezo wa wanadamu.”

Je, kujihusisha na mambo ya uchawi au kuwasiliana na pepo ni burudani isiyokuwa na madhara?