Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Akili Zilizovurugika

Akili Zilizovurugika

Akili Zilizovurugika

NICOLE amekuwa akishuka moyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 14. Hata hivyo, alipokuwa na umri wa miaka 16, alianza kuhisi tofauti—alisisimuka kupita kiasi na kuhisi ana nguvu nyingi mno. Aliwaza sana, alisema mambo yasiyoeleweka, alikosa usingizi na kushuku kwamba marafiki wake wanamtumia ili kujifaidi. Kisha, Nicole alidai kwamba angeweza kubadilisha rangi ya vitu. Hapo ndipo mama yake alipotambua kwamba Nicole anahitaji kumwona daktari, kwa hiyo akampeleka hospitalini. Baada ya kumchunguza, madaktari wakagundua kwamba Nicole ana ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika. *

Kama Nicole, mamilioni ya watu ulimwenguni pote wana ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika au ugonjwa wa kushuka moyo. Magonjwa hayo yanaweza kusababisha madhara makubwa mno. Steven anayeugua ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika anasema: “Nilifadhaika kwa miaka mingi, nilishuka moyo na wakati mwingine nikasisimuka kupita kiasi. Matibabu yalisaidia, lakini bado nilifadhaika.”

Ni nini kinachosababisha magonjwa ya kihisia? Watu walioshuka moyo au wenye ugonjwa wa hisia zinazobadilika-badilika hukabili magumu gani? Wagonjwa na wale wanaowatunza wanaweza kusaidiwaje?

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 2 Baadhi ya dalili zilizotajwa zinaweza pia kuwa dalili za ugonjwa wa akili, matumizi ya dawa za kulevya, au hata mabadiliko yanayotukia wakati wa kubalehe. Ugonjwa unaweza kutambuliwa tu baada ya kuchunguzwa kikamili na mtaalamu.