Jani Lisilolowa Maji la Yungiyungi
Je, Ni Kazi ya Ubuni?
Jani Lisilolowa Maji la Yungiyungi
▪ Eti vikombe vya plastiki vinavyojisafisha vyenyewe, madirisha yasiyopata maji wakati wa mvua, mashini ndogo sana zinazofanya kazi bila kusuguana? Wanasayansi wanasema kwamba hizo ni baadhi tu ya faida tunazoweza kupata kwa kutumia muundo wa jani la yungiyungi.
Fikiria hili: Sehemu ya juu ya jani la yungiyungi lina mabonge madogo sana ambayo yamefunikwa kwa fuwele zenye nta. Matone ya maji yanapoanguka juu ya majani hayo yanakwama kwenye mirija hiyo ambayo huzuia jani lisilowe maji. Mwinamo wa jani hufanya maji yamwagike hata kabla hayajagusa sehemu ya juu ya jani. Matokeo ni nini? Jani la yungiyungi halilowi maji na pia linadumu likiwa safi kwa kuwa uchafu na vumbi husafishwa na maji hayo.
Wanasayansi wanataka kubuni vitambaa ambavyo havilowi maji kamwe kwa kuiga jani la yungiyungi. Hata mashini ndogo sana, ambazo zinaweza kuharibiwa na maji zitafaidika na muundo huo wa jani la yungiyungi. “Kuna njia nyingi sana za kutumia [muundo wa jani hilo],” linaripoti gazeti Science Daily.
Una maoni gani? Je, jani la yungiyungi lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?