Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 1

Sifa za Yehova

Sifa za Yehova

(Ufunuo 4:11)

  1. 1. Yehova Mungu, Mwenye Uwezo,

    Muumba wetu, mwenye enzi kuu.

    Uumbaji wakusifu wewe;

    Unaonyesha nguvu zako.

  2. 2. Hukumu zako zote za haki.

    Uadilifu, unatufundisha.

    Neno lako tunapolisoma,

    Hekima yako, twaiona.

  3. 3. Upendo wako, ni sifa kuu.

    Zawadi zako, hazina kifani.

    Jina lako, nazo sifa zako,

    Twazitangaza kwa furaha.