Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 94

Kulithamini Neno la Mungu

Kulithamini Neno la Mungu

(Wafilipi 2:16)

  1. 1. Ee, Yehova Baba, twakushukuru,

    Kwa kutupa Neno lako la nuru!

    Roho iliongoza,

    walioandika.

    Latupa hekima, twawekwa huru.

  2. 2. Neno lina nguvu, lapenya moyo.

    Linatambua fikira na nia.

    Sheria zako njema,

    na ni kamilifu.

    Zaturekebisha, zatuongoza.

  3. 3. Nalo Neno lako, latuvutia.

    Manabii walilizingatia.

    Tujifunzapo Neno,

    Tunaimarishwa;

    Tunakushukuru, kwa Neno lako!