Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 152

Mahali Panapokutukuza

Mahali Panapokutukuza

(1 Wafalme 8:27; 1 Mambo ya Nyakati 29:14)

  1. 1. Yehova, Muumba wa Mbingu,

    Mbinguni hakukutoshi,

    Sembuse basi jengo hili.

    Ila roho yako ipo.

    Wanaotumikia hapa,

    Umewapa nuru yako.

    Twafanya kazi kwa umoja;

    Twakutukuza Yehova.

    (DARAJA)

    Hatuna chochote

    Kisichotoka Kwako.

    Vyote tunavyokupa

    Vimetoka kwako.

    (KORASI)

    Twauthamini wema wako;

    Nyimbo za sifa twaimba.

    Umetimiza ndoto yetu

    Kwa kutupa jengo hili.

  2. 2. Yehova, umetupatia

    Mahali pa kukusifu,

    Pahudumie watu wako,

    Na wengine wakujue.

    Kusudi lako litimie.

    Bado kuna kazi nyingi,

    Ya kuendeleza huduma

    Aliyotupa Mwanao.

    (DARAJA)

    Basi tunakupa

    Vyote vilivyo bora.

    Ni Wewe wastahili,

    Kupokea sifa.

    (KORASI)

    Twauthamini wema wako;

    Nyimbo za sifa twaimba.

    Umetimiza ndoto yetu

    Kwa kutupa jengo hili.