Hamia kwenye habari

Miradi ya Wallkill na Warwick Inaendelea Kutekelezwa

Miradi ya Wallkill na Warwick Inaendelea Kutekelezwa

Miradi miwili muhimu ya ujenzi ya Mashahidi wa Yehova nchini Marekani inaendelea kutekelezwa, tunawashukuru sana wajitoleaji ambao wanatoka maeneo mbalimbali nchini Marekani.

Wallkill, New York: Mashahidi 1,600 wanaishi katika majengo haya na ndio kitovu cha uchapishaji wa machapisho ya Mashahidi wa Yehova nchini Marekani. Wajenzi ​—ambao wengi wao ni wajitoleaji​—wanaendelea kufanya kazi ya kuongeza idadi ya majengo, na sasa wanajenga jengo jipya lenye ghorofa tatu ambalo litakuwa na ofisi, maegesho ya magari, na jengo lenye ghorofa tatu kwa ajili ya makazi ya wafanyakazi. Hadi kufikia mwaka 2012, wajitoleaji walikuwa wamemaliza kujenga jengo la kuhifadhia vifaa mbalimbali vya kiufundi na mahali pa kulia chakula pameongezwa kwa ajili ya watu 200 zaidi.

Mashahidi wa Yehova wana ofisi mbalimbali zinazosimamia utendaji wao katika nchi nyingi, zinajulikana kwa jina la ofisi za tawi, nazo zinatia ndani Brazili, Ujerumani, na Mexico. Nchini Marekani, majengo ya Mashahidi wa Yehova yanatia ndani kituo cha elimu kilichopo Patterson, New York, na ofisi zilizo Brooklyn, New York. Upanuzi huo utakapokamilika, majengo ya Wallkill ndiyo yatakayokuwa makubwa zaidi kuliko majengo yote ya Mashahidi wa Yehova ulimwenguni.

Warwick, New York: Hapa ndipo patakapokuwa makao makuu mapya ya ulimwenguni pote ya Mashahidi wa Yehova. Picha ya majengo hayo imeondolewa kwenye tovuti. Mashahidi wamenunua kiwanja ambacho kipo umbali wa kilomita 10 (maili 6), katika eneo la Tuxedo, New York, ili wahifadhi vifaa vya ujenzi. Wenye mamlaka katika eneo hilo wameikubali ripoti ya mwisho inayoonyesha athari za mazingira zinazoweza kusababishwa na mradi huo wa ujenzi. Mara tu mpango wa ujenzi utakapoidhinishwa, basi tutatuma maombi ili kuomba vibali vya kuanza kujenga. Kwa wakati huu, bado makao makuu ya ulimwenguni pote ya Mashahidi wa Yehova yataendelea kuwa Brooklyn, New York.