Hamia kwenye habari

Mvua kubwa ilisababisha mafuriko na uharibifu mkubwa katika jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini

APRILI 25, 2022
AFRIKA KUSINI

Mvua Kubwa na Maporomoko ya Ardhi Yasababisha Uharibifu Nchini Afrika Kusini

Mvua Kubwa na Maporomoko ya Ardhi Yasababisha Uharibifu Nchini Afrika Kusini

Aprili 13, 2022, mvua kubwa ilipiga baadhi ya maeneo ya jimbo la KwaZulu-Natal la Afrika Kusini na kusababisha vifo vya mamia ya watu na uharibifu mkubwa. Katika baadhi ya maeneo kiwango cha mvua kilifikia milimita 300 katika muda wa saa 24. Maeneo mengi yalibaki bila maji na umeme. Barabara nyingi zimeharibika.

Athari ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa

  • Binti ya dada mmoja alipata majeraha madogo baada ya kuangukiwa na ukuta

  • Ndugu mmoja alipata majeraha madogo nyumba yake ilipoharibiwa

  • Nyumba 27 zimeharibiwa kabisa

  • Nyumba 102 zimepata uharibifu mdogo

  • Wahubiri 87 wamelazimika kuhama makao yao

  • Majumba 2 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada imeundwa ili kupanga kazi ya kutoa msaada

  • Wazee wa makutaniko na waangalizi wa mzunguko wanawapa wahubiri msaada unaohitajika

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinatolewa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya COVID-19

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza ndugu zetu wapendwa ambao wanateseka kwa sababu ya msiba uliowapata, huku tukisubiri kupata baraka za milele alizoahidi.​—2 Wakorintho 4:18.