Hamia kwenye habari

FEBRUARI 2, 2017
CHILE

Mioto ya Misitu Nchini Chile

Mioto ya Misitu Nchini Chile

Mashahidi wa Yehova wanawasaidia waamini wenzao pamoja na watu wengine walioathiriwa na mioto ya msitu inayozidi kuenea katika maeneo ya katikati na kusini mwa Chile. Kufikia sasa mioto hiyo imeharibu eneo lenye ukubwa wa ekari milioni 1.2. Wenye mamlaka wanasema kwamba mioto hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kwa majuma mawili, ni mojawapo ya mioto mibaya zaidi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Chile inaripoti kwamba hakuna Mashahidi ambao wamejeruhiwa au kufa kutokana na mioto hiyo. Wengine kati yao walihitaji kuhamishwa kutoka katika eneo hilo na wanaishi na waabudu wenzao.

Nyumba tano za Mashahidi wa Yehova ziliharibiwa na mioto hiyo. Ofisi ya tawi ilianzisha halmashauri ya kutoa msaada ili kuchanganua ni mambo gani mengine yanayohitaji kushughulikiwa na mpango wa kutoa msaada.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia kazi ya kutoa msaada wakati wa misiba kutoka kwenye makao yao makuu ya ulimwenguni pote, kwa kutumia michango iliyotolewa kwa ajili ya kazi ya kuhubiri ulimwenguni pote ya Mashahidi.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Chile: Jason Reed, +56-2-2428-2600