Hamia kwenye habari

MEI 12, 2023
SUDAN

Mapigano Makali Yaendelea Nchini Sudan

Mapigano Makali Yaendelea Nchini Sudan

Aprili 15, 2023, mzozo ulizuka baina ya vikundi viwili vyenye silaha Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Ripoti za habari zinaonyesha kwamba mzozo huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya 600 huku wengine 5,000 wakiwa wamejeruhiwa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Ndugu na dada waliokimbia mzozo jijini Khartoum, wakutanika kwa usalama katika jiji la Wad Madani, nchini Sudan ili kupata faraja ya kiroho

    Hakuna ndugu au dada yetu aliyejeruhiwa au kufa

  • Karibu wahubiri 318 wamelazimika kuhama makao yao. Baadhi yao wamekimbilia nchi jirani na wamefika salama

  • Kwa muda fulani watu 8 hakuweza kuondoka katika sehemu yao ya kazi na watoto 5 hakuweza kuondoka shuleni. Kwa sasa wote wameungana tena na familia zao

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Wazee wa eneo hilo wanawategemeza kiroho wahubiri walioathiriwa

  • Halmashauri za Kutoa Msaada zimewekwa rasmi nchini Sudan na katika nchi jirani ili kusimamia jitihada za kutoa msaada na pia kuandaa mahitaji mbalimbali

Tutaendelea kusali kwa ajili ya ndugu zetu ambao maisha yao yamevurugwa na machafuko yanayoendelea tukisubiri kwa hamu wakati unaokuja ambapo “amani itakuwa nyingi.”​—Zaburi 72:7.