Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mdomo wa Toucan

Mdomo wa Toucan

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mdomo wa Toucan

▪ Kwa kuwa hawezi kupaa vizuri, ndege anayeitwa toucan wa Amerika ya Kati na ya Kusini husonga kwa kuruka-ruka. Toucan wa jamii fulani hutoa mlio unaofanana na ule wa chura lakini kwa nguvu zaidi. Sauti yake inaweza kusikika umbali wa kilomita moja hivi. Hata hivyo, jambo ambalo linawashangaza wanasayansi zaidi kuhusu ndege huyo ni mdomo wake.

Fikiria hili: Urefu wa mdomo wa toucan fulani ni karibu nusu ya ndege mwenyewe. Unaonekana mzito lakini ni mwepesi. “Sehemu yake ya juu imefanyizwa kwa keratini kama ile inayotengeneza kucha na nywele,” anaeleza mwanasayansi Marc André Meyers. “Ni kama matabaka mengi ya vipande vyembamba vyenye pembe sita, vinavyolaliana kama mbao zilizoezeka paa.”

Ugumu wa mdomo wa ndege huyo umelinganishwa na sifongo ngumu. Sehemu fulani za mdomo huo si pana sana huku sehemu nyingine zimefanyizwa kwa vitu vigumu. Kwa sababu hiyo mdomo huo ni mwepesi lakini una nguvu za ajabu. “Ni kana kwamba toucan ana ujuzi mwingi sana kuhusu ufundi,” anasema Meyers.

Muundo wa mdomo wa toucan humwezesha kukabiliana anapogongwa kwa nguvu. Wanasayansi wanaamini kwamba muundo wa mdomo huo unaweza kuigwa na wajenzi wa ndege na magari. “Mabati yaliyoundwa kama mdomo wa toucan yanaweza kuwalinda zaidi abiria wakati wa aksidenti,” anasema Meyers.

Una maoni gani? Je, mdomo wenye nguvu lakini mwepesi wa toucan ulijitokeza wenyewe? Au je, ulibuniwa?

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 17]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Sehemu ya ndani ambayo si pana

Muundo kama wa sifongo