Hamia kwenye habari

Awamu ya 6 ya Picha za Uingereza (Machi Hadi Agosti 2018)

Awamu ya 6 ya Picha za Uingereza (Machi Hadi Agosti 2018)

Katika awamu hii ya picha, utaona jinsi ujenzi ulivyoendelea katika ofisi mpya ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Uingereza kati ya Machi na Agosti 2018.

  1. Jengo la Kaskazini la Uzalishaji

  2. Jengo la Kusini la Uzalishaji

  3. Jengo la Ofisi

  4. Makazi A

  5. Makazi B

  6. Makazi C

  7. Makazi D

  8. Makazi E

  9. Makazi F

Machi 8, 2018—Eneo la Ujenzi wa Ofisi ya Tawi

Mshiriki wa kikosi cha kushughulikia mazingira akipima kiwango cha asidi kwenye maji kutoka kwenye dimbwi la kupunguza mafuriko lililo karibu na mwingilio mkuu. Ukaguzi huo unahakikisha kwamba hatua zinazochukuliwa kudhibiti vitu vinavyochafua maji zinafanya kazi.

Machi 13, 2018—Makazi B

Dada akizoezwa kuweka mbao zisizoathiriwa na hali zinazobadilika za hewa. Pamoja na vitu vinavyotumiwa kuzuia hewa, joto, au baridi kuathiri nyaya, na matofali madogo, mbao hizo zinafanyiza ukuta wa nje wa makazi.

Aprili 5, 2018—Jengo la Kusini la Uzalishaji

Mashine inayotumiwa kukandamiza barabara kabla ya kumwaga lami. Sehemu hii ya barabara kando ya Jengo la Kusini la Uzalishaji inazunguka eneo lote la ofisi.

Mei 1, 2018—Jengo la Ofisi

Picha ya angani kutoka upande wa kaskazini mashariki. Kreni iliyo hapo mbele iko kwenye eneo la mapokezi la jengo la ofisi. Upande wa kulia ni sakafu iliyotayarishwa ya Jengo la Ofisi, na upande wa kushoto ni msingi wa jikoni, chumba cha kulia chakula, na ukumbi. Sehemu ya wageni kutazama imehamishwa ili waweze kuona ujenzi vizuri.

Mei 9, 2018—Jengo la Ofisi

Mihimili ya paa ikiingizwa katika sehemu zake, ni sehemu ya jikoni, chumba cha kulia chakula, na ukumbi wa jengo la ofisi.

Mei 14, 2018—Jengo la Ofisi

Mshiriki wa kikosi cha kushughulikia mazingira akiangalia jinsi uchimbuaji unavyofanywa karibu na mti usiopaswa kuharibiwa. Wachimbuaji wanazuia madhara kwa kuweka vizuizi kandokando ya mizizi ya mti huo. Miti fulani inahifadhiwa kwa eneo lenye mizizi kuzungushiwa ua na ujenzi hauruhusiwi katika maeneo hayo.

Mei 24, 2018—Makazi E

Mfanyakazi akipanda maua kandokando ya njia ya mguu. Vijiti vitasaidia maua kubaki kwenye sehemu zilizopandwa huku mizizi ikikua.

Juni 19, 2018—Makazi D

Mpaka-rangi akiweka namba ya utambulisho kwenye mbao ya kurembesha itakayowekwa kwenye gorofa ya tatu. Mwezi uliofuata, wajenzi walianza kuhamia kwenye Makazi D.

Juni 20, 2018—Jengo la Ofisi

Wanakandarasi wakishusha ngazi za saruji kwenye sehemu yake.

Juni 26, 2018—Jengo la Ofisi

Washiriki wa kikosi cha kutengeneza kuta zinazotokana na chokaa ngumu wakiunganisha fremu ya ukuta kwenye dari. Upande wa kulia ni kifaa cha kuinua kinachotumiwa na kikosi cha mfumo wa HVAC wanapoweka viyoyozi.

Julai 10, 2018—Jengo la Ofisi

Washiriki wa kikosi cha mfumo wa maji wakiweka vitu vya kushikilia mabomba chini ya eneo la mapokezi la jengo la ofisi.

Julai 10, 2018—Majengo ya Uzalishaji

Wafanyakazi wakichimba mifereji kati ya Jengo la Kaskazini la Uzalishaji na Jengo la Kusini la Uzalishaji.

Julai 17, 2018—Jengo la Ofisi

Wanakandarasi wakiweka sehemu ya mwisho ya varanda nje ya chumba cha kulia chakula. Sehemu ya chini inaelekea kwenye Makazi A.

Julai 19, 2018—Jengo la Kusini la Uzalishaji

Boriti za chuma zinawekwa. Jengo hili litakuwa na karakana na ofisi.

Agosti 2, 2018—Eneo la Ofisi ya Tawi

Picha ya angani kutoka upande wa kaskazini magharibi. Upande wa kati kulia, fremu ya chuma ya Jengo la Kusini la Uzalishaji imekamilika na ukuta umeanza kujazwa. Upande wa mbele, kazi imeanza katika Jengo la Kaskazini la Uzalishaji, na sehemu ya chini yenye lami imewekwa. Upande wa kati kushoto kuja jengo la ofisi, na jengo la makazi pia linaonekana nyuma.

Agosti 3, 2018—Makazi

Picha ya angani kutoka upande wa mashariki wakati wa mapambazuko. Upande wa mbele, Makazi D, E, na F yamekamilika. Makazi C yamepangwa kukamilika mwezi wa Oktoba.

Agosti 7, 2018—Jengo la Ofisi

Wakitumia mawe ya chokaa, wafanyakazi wanajenga ukuta kando ya kidimbwi. Eneo hili litakuwa mwingilio wenye kuvutia wa jengo la ofisi, linaloonekana nyuma kupitia miti.

Agosti 7, 2018—Jengo la Ofisi

Maseremala wakiweka vifaa vya HVAC na vya umeme kwenye dari ya ofisi. Ofisi hii inatumiwa kusaidia kazi mbalimbali kufanywa kwa utaratibu unaofaa.

Agosti 21, 2018—Jengo la Ofisi

Kuta za Jengo la Ofisi zimeanza kusimamishwa. Kutumia mabamba ya kuta yaliyotayarishwa mapema kunasaidia kuharakisha kazi ya ujenzi, hivi kwamba kufikia mwishoni mwa Agosti, Jengo la Ofisi litakuwa na kuta zake zote. Madirisha makubwa yanaruhusu mwanga mwingi iwezekanavyo ndani ya ofisi. Madirisha yametengenezwa kwa njia ya kwamba hayaruhusu mwanga mkali wa jua katika majira ya baridi kali wala joto linalotokana na jua katika majira ya kiangazi.

Agosti 24, 2018—Jengo la Ofisi

Wafanyakazi wakijitayarisha kufunika chuma za paa juu ya chumba cha kulia chakula na ukumbi. Kuta hizo zitapunguza kiasi cha sauti wakati ambapo maeneo yote mawili yanatumika wakati uleule.