Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY

Sakinisha JW Library Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Android

Sakinisha JW Library Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Android

Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library kwenye kifaa chako cha Android kutoka kwenye app store, kama vile Google Play Store au Amazon Appstore, unaweza kuisakinisha kwa kutumia JW Library Android package (APK).

Ili kusakinisha JW Library APK, utahitaji kukiruhusu kifaa chako kiweze “kusakinisha programu zisizojulikana” au “kuruhusu programu kutoka vyanzo visivyojulikana ziwekwe.” Ili kujua jinsi ya kufanya hivyo, soma kitabu cha mwongozo cha kifaa chako cha Android.

Fuata hatua hizi ili kupakua na kusakinisha JW Library APK:

  1. Bofya kitufe cha Pakua kilicho kwenye ukurasa huu, kisha uhifadhi programu ya APK uliyopakua kwenye kifaa chako.

  2. Tafuta programu hiyo ya APK katika kifaa chako, kisha ibofye ili usakinishe JW Library.

Baada ya kusakinisha JW Library APK, angalia mara kwa mara ikiwa kuna toleo jipya la programu hiyo. Ili kufanya hivyo, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua ukurasa wa Mipangilio kwenye JW Library ili kujua toleo unalotumia.

  2. Ikiwa namba ya toleo unalotumia ni tofauti na namba iliyo hapo chini kwenye kifaa chako, pakua na kusakinisha faili ya APK kwa kufuata hatua zilizotajwa hapo juu.

Version: 14.3 (408605)