Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Nitainuka

Nitainuka

Pakua:

  1. 1. Nimechoka nalemewa na upweke.

    Yehova, naona kosa langu.

    Nimeshuka moyo, ninahitaji nguvu.

    Natamani hali ya awali.

    (KORASI)

    Nazikumbuka vizuri​—⁠sheria zako​—

    Kweli muhimu za Neno lako.

    Hata nikijikwaa, na kuanguka,

    Nitainuka.

  2. 2. Najua wananipenda,

    Na wananijali,

    Wanaompenda Yehova.

    Neno lako ni ta’ laniongoza kurudi.

    Nataka kubaki kwenye njia.

    (DARAJA)

    Hata niende, wapi siwezi, kusahau kweli:

    Mwisho u karibu.

    (KORASI)

    Yehova, tafadhali sala sikia

    Nisaidie nasononeka.

    Wajua nikijikwa’ mara nyingi,

    Nitainuka.

    (DARAJA)

    Yehova anaelewa; nahitaji msaada.

    Anijua vizuri kuwa mi ni dhaifu.

    Anaona mema kwangu.

    (KORASI)

    Leo naenda mkutano nihisi upendo,

    Nilipokuwa awali.

    Hata nikijikwaa, na kuanguka, Nitainuka.

    Nitainuka.